Serikali imeliagiza Shirika la Maendeleo ya Taifa NDC kulipa deni lakiasi cha shilingi bilioni 4.5 baada ya kuingia mkataba wa mkopo waliokopeshwa na Shirika la Hifadhi ya Jamii NSSF, ili kujenga kiwanda cha kimkakati cha kutengeneza viuadudu vya Malaria cha TBPL kilichopo Kibaha Mkoani Pwani.
Aidha uwepo wa deni hilo ambalo NDC wameshindwa kulilipa hadi kufikia kiasi cha Bilioni 8 hali ambayo imeathiri uzalishaji kiwandani hapo na kutishia ajira za wafanyakazi 89 waliopo.
Akizungumza baada ya kutembelea kiwanda hicho Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama ameitaka NDC kukaa chini na NSSF ili kuangalia namna bora ya kulipa mkopo huo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa NSSF, Gabriel Silayo amesema lengo la Shirika lake ni kuinua uchumi wa taifa na wanachama kwa ujumla.
Hali kadhalika wanasheria wa NDC Henry Bakaru ameahidi kufanyia kazi maagizo yaliyotolewa na Waziri Mhagama.