Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Zambia na klabu ya Zanaco Moses Phiri amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu usajili wake ndani ya Simba SC.

Phiri ambaye kwa kipindi cha majuma kadhaa amekua akihusihwa na mpango wa kusajiliwa Msimbazi, amesema suala hilo lipo na linaendelea vizuri.

Amesema kiu yake ni kucheza Soka nje ya Zambia, na anaamini Tanzania ni sehemu sahihi, tena itampendeza kama atakamilisha mpango wa kutua kwa Mabingwa Simba SC.

“Ni kweli suala la kuja Simba lipo, kwa upande wangu sina kipingamizi kwani Simba ni timu kubwa na litakuwa jambo kubwa kwangu kucheza Simba na nitajitahidi kuonyesha kiwango bora kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu.”

“Dhamira yangu kwa sasa ni kucheza nje ya Zambia, na Tanzania ninaona ni mahala sahihi pa kuanzia ndoto yangu.”

Bado inadaiwa kuwa usajili wa Kiungo huyo Mshambuliaji, utategemea kuondoka kwa Luis Miquissone ambaye anawaniwa na klabu kadhaa za Afrika ya Kaskazini.

Euro 2020: Mashabiki waiponza England
Deni la NDC lafikia Bilioni 8