Dhamira ya dhati ya Rais, Samia Suluhu Hassan ya kuitazama kwa karibu sekta ya kilimo, ikiwemo kuongeza bajeti ya Wizara Kilimo, kutoka sh. Bilioni 254 mwaka wa fedha 2021/2022 hadi sh bilioni 954 kwa 2022/2023, italeta mabadiliko katika uchumi wa Taifa.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka Mkoani Morogoro na kuongeza kuwa miongoni mwa mabadiliko hayo ni pamoja na kutengeneza fursa nyingi za ajira.

Amesema, Rais Samia ametenga Sh. bilioni 954 ukilingalisha na bajeti ya mwaka 2021/2022 ya Sh. bilioni 254 ambazo ni karibia asilimia 224 ya ongezeko hilo la bajeti ambayo itasaidia kutatua changamoto ya ajira kwa vijana hasa wasomi wa vyuo vikuu ambao ametaka watambuliwe na kuwezeshwa kupitia kilimo.

Shaka ameongeza kuwa, “Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi imeahidi katika kipindi cha miaka mitano tutazalisha ajira milioni nane kwa Watanzania, sasa kwenye kutafsiri maelekezo ya Ilani Serikali ya Rais Samia imeshajiwekea mwelekeo ama imeshajiwekea matatarajio yake katika ajira hizo.”

Aidha, amebainisha kuwa Serikali inatarajia hadi kufikia 2025 karibia ajira milioni tatu zitakuwa zimezalishwa kupitia sekta ya kilimo, huku akisema hatua hiyo ni mageuzi chanya na ni ukombozi kwa vijana na wanawake nchini.

Waziri Mstaafu afarijika kumuona Rais msibani
Wawili wafa kwa radi nje ya Ikulu