Nyota wa muziki wa bongo fleva Diamond Plutnumz amefunguka kuwa ngoma yake na Rick Ross itatoka tarehe 1 mwezi Desemba mwaka huu.

Akifanya mahojiano na mtangazaji wa kituo cha televisheni cha BBC, Salim Kikeke nchini Uingereza Diamond amesema wimbo huo unaoitwa Waka utakuwa kwenye albamu yake mpya inayoitwa ‘A boy From Tandale’ ambayo pia itatoka mwezi Desemba.

Katika albam hiyo yenye nyimbo 18, Diamond ambaye anatamba na wimbo wake wa Allelujah amesema amewashirisha wasaniii tofauti wa hapa Tanzania na wasanii wengine wa kimataifa kama Davido, Omarion, Rick Ross na wengine wengi.

 

 

 

 

Watumishi wa umma watakiwa kujitathmini
Sadio Mane aipeleka Senegal kombe la dunia