Diamond Platinumz ni mmoja kati ya watu walioguswa zaidi na msiba wa mwanamuziki nguli, Papa Wemba kwani alikuwa ameshafanya naye mradi uliokuwa ukiiva studio.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Diamond ameeleza jinsi alivyofanya kazi na mwimbaji huyo hivi karibuni alipokuwa mapumzikoni jijini Paris, Ufaransa.

“Wiki nne tu zilizopita tulikuwa Paris, akanishirikisha kwenye nyimbo yake, tukapanga mengi juu ya wimbo halafu ghafla naskia habari ya msiba…Dah! nimesikitika sana. Hakika binadamu ni wazungumzaji tu ila Mwenyez Mungu ndiyo mpangaji…Pumzika salama Kiongozi wetu daima tutakukumbuka,” Diamond aliandika.

Papa Wemba alifariki Jumapili iliyopita baada ya kuanguka ghafla akiwa jukwaani nchini Ivory Coast.

Jenerali wa Jeshi la Burundi na Mkewe wauawa
TFF Yaingilia Kati Sakata La Uchaguzi Wa Young Africans