Mshambuliaji Diego Costa ameondolewea kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Hispania ambacho itacheza michezo miwili ya kimataifa.

Hispania itacheza mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia dhidi ya Macedonia kwenye mji wa Granada siku ya jumamosi, na katikati ya juma lijalo itakaribishwa jijini London kwenye uwanja wa Wembley kupambana na England katika mpambano wa kimataifa wa kirafiki.

Mshambuliaji huyo wa klabu ya Chelsea amelazimika kuondoka katika kambi ya Hispania baada ya kuumia nyonga.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Hispania Julen Lopetegui alikua na matarajio makubwa na mshambuliaji huyo kuuwahi mchezo dhidi ya England, lakini kitengo cha utabibu kimetoa uthibitisho wa majibu ya vipimo alivyofanyiwa Costa na kubaini jambo hilo halitowezekana.

Azam FC Kusuka Kikosi Cha Nguvu Raundi Ya Pili
Alexis Sanchez Kurejeshwa London