Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, jana alimtembelea Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad kwa lengo la kumjulia hali akiwa amepumzika katika hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.

Dk Shein na Maalim Seif

Rais Shein aliambatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Utawala Bora, Dk. Mwinyihaji Makame ambapo walifanya mazungumzo na Maalim Seif ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF).

Ziara hiyo ya Rais Shein aliwasili katika hotel hiyo majira ya saa mbili usiku ikiwa ni saa chache baada ya Rais John Magufuli kumtembelea mwanasiasa huyo mkongwe.

Maalim Seif alieleza kuwa hali yake inaendeelea kuimarika zaidi na kuwashukuru Marais hao kwa nyakati tofauti.

Maalim Seif na Dk. Shein

Polisi Zanzibar Yatamba Kutetea Taji Lao Uganda
Ajabu: Apewa ujauzito na wanaume wawili, azaa mapacha wa baba tofauti