Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein leo anatarajiwa kufungua Baraza la Wawakilishi visiwani humo akiwa na kitendawili cha kumpata Makamu wa Kwanza wa Rais.

Dk. Shein ambaye aliibuka mshindi kwenye uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20 mwaka huu uliosusiwa na vyama kadhaa vya upinzani ikiwa ni pamoja na chama kikuu cha upinzani cha CUF, kwa kupata zaidi ya asilimia 90 ya kura zilizohesabiwa, anakabiliwa na kitendawili cha kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kwani hakuna chama kilichopata asilimia 10 katika uchaguzi huo kama inavyoelekezwa na Katiba.

Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010 ilianzisha SUK inayomtaka Rais kuchagua Makamu wa Kwanza wa Rais kutoka chama cha upinzani kilichopata angalau asilimia 10 ya kura zote.

Kulingana na hali hiyo, Rais Shein anachangamoto kwani kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar hataweza kuchagua nusu ya Baraza la Mawaziri kutoka Upinzani wala Makamu wa Kwanza.

Hata hivyo, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd alieleza kuwa ni lazima Rais Shein ataunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Kitendawili kinchosubiriwa kutenguliwa ikiwa ni siku moja baada ya CUF kutoa maazimio yake 13, moja likiwa ni kutomtambua Rais Shein pamoja na Serikali yake.

Kamati ya Bunge yaibana TCRA kwa kutumia mabilioni kujilipa posho na safari
Tajiri Wa Kiarabu Kuiongoza African Lyon