Chuo cha Taaluma ya Polisi Dae es salaam – DPA, kimeendelea kutoa elimu na mafunzo
mbalimbali kwa maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali katika kukabiliana na majanga
ya moto pindi yanapotokea.

Akitoa taarifa hiyo leo Mei 30,20223 Mkuu wa chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam
kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Dkt. Lazaro Mambosasa amesema kuwa chuo
hicho kimekuwa na utaratibu wa kutoa elimu kwa wanafunzi wa kozi mbalimbali wawapo chuoni
hapo.

Ameendelea kueleza kuwa lengo la kutoa elimu hiyo ni kujenga uwezo kwa maofisa,wakaguzi
na askari wa vyeo mbalimbali wa Jeshi hilo na makundi mengine ya wahitaji ambapo
amebainisha kuwa ni vyema kila askari kuwa na vifaa wezeshi ili kukabiliana na majanga hayo
pindi yanapotokea.

Mbali na hilo Mkuu wa chuo hicho ametumia fursa hiyo kumpa pole mkufunzi wa chuoni hapo
aliyepata majanga ya kuunguliwa moto nyumba yake, ambapo amebainisha kuwa kutokana na
changamoto hiyo aliyoipata waliona vyema kuungana kama Jumuiya ya Chuo cha Taaluma ya
Polisi kumpa Mkono wa Pole kwa kadhia aliyoipata.

Kwa upande wake Sajenti Saidi Hamad aliyepata janga hilo la kuunguliwa moto nyumba yake
ameushukuru uongozi wa chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam kwa namna walivyoguswa
na tukio hilo, ameongeza kuwa nyumba yake iliyopo Zanzibar iliteketea yote kwa moto ambapo
anamshukuru Mungu familia imebaki salama.

Hatma ya Minziro, Wandiba kujulikana leo
Bosi FC Barcelona aweka wazi usajili wa Messi