Kila mmoja huchagua kuishi kwa kutumia mifumo itakayomfanya kuwa huru na mwenye amani kwenye maisha yake ili kuishi vile anavyohitaji.

Wakati mamilioni ya watu wa karne hii ya 21 huonyesha wazi kutekwa kiasi cha kushindwa kuishi hata nusu ya siku bila kutumia simu zao za mikononi, hilo limekuwa tofauti kwa mwanamuziki hodari kutoka nchini Uingereza Edward Christopher Sheeran maarufu Ed Sheeran (30).

Yeye ameweka wazi kuwa hajaigusa wala kuitumia simu yake ya mkononi kwa takribani miaka saba tangu mwaka 2015.

Ed sheeran ameyasema hayo kupitia kwenye mahojiano yake na ‘Collector’s Edition podicast’ ambapo alibainisha kuwa hatumii simu kwa kuwa ilikuwa kama sehemu ya kuharibu afya yake ya akili.

“Nilikuwa kama napata mzigo mzito hivi na huzuni nikiwa na simu yangu, natumia muda wangu kwa uchache sana, kitendo cha kuiacha simu nilikuwa ni kama nimekatia mahusiano na watu, kwa sasa natumia email pekee na ni kwa siku chache sana nikipata muda natumia Laptop yangu kujibu email walau kumi pekee kwa muda huo kisha narudi kuishi maisha yangu.” alisema.

Kocha Simba SC aomba radhi
Haji Manara kuhama Tanzania