Mshambuliaji wa Kimataifa wa Simba SC, Emmanuel Okwi anaendelea vizuri kutoka kwenye majeraha aliyoyapata kwenye mchezo wa jana dhidi ya Mbao FC.

Daktari wa kikosi cha Simba, Yassin Gembe amesema mchezaji huyo tayari ameshapatiwa tiba na kuna uwezekeno mkubwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachoivaa Stand United Ijumaa wiki hii kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Okwi anaendelea vizuri sana tofauti na jana, kwa hali aliyonayo pamoja na tiba ambazo tumeshampatia ni asilimia kubwa sana kwa yeye kuwepo kwenye mchezo unaofuata dhidi ya Stand United Ijumaa hii,” amesema Gembe.

Wakati huo huo Mshambuliji wa timu ya Mbao FC, Habib Kiyombo amesema moja ya sababu iliyopelekea kupokea kipigo kikubwa cha mabao 5-0 kutoka kwa jana Simba ni kuzidiwa uzoefu.

Mbao ilicheza mechi yake ya kwanza tangu kupanda ligi kuu msimu uliopita katika uwanja wa mkuu wa Taifa ambao eneo lake la kuchezea ni kubwa kulinganisha na viwanja vingi zinavyochezewa ligi.

Kiyombo ambaye anakumbukwa kwa kufunga mabao yote mawili katika ushindi dhidi ya Yanga kwenye uwanja wa CCM Kirumba amesema Simba waliwazidi ujanja karibia kila sehemu.

Video: Wanaharakati wa haki za binadamu kuishtaki serikali
Kamati ya maadili ya TFF yawafungia wadau kwa kughushi leseni