Waziri wa Mali Asili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema kuwa baioanuwai kwenye eneo la mita 3500, la Mlima Kilimanjaro ambalo lina aina chache ya wanyama linakadiriwa kuharibika. kufuatia mlipuko wa moto uliozuka juzi Oktoba 11,2020.
Kingwangalla ametumia ukurasa wake wa twitter kueleza namna ambavyo serikali inepambana kukabiliana na janga hilo la moto.
“Moto huu utakuwa umeharibu baioanuwai kwenye eneo la mita kati ya 2000 na 3500, ambayo ni Alpine region yenye vichaka na aina chache sana za wanyama,” ameandika Kigwangalla.
aidha Kigwangalla amesema kuwa hadi kufikia sasa timu ya watu 500 ipo eneo la tukio kudhibiti moto usiendelee kuleta madhara makubwa.
“Tumeshinda vita/maadui wengi wagumu kwa sala na dua zetu, naamini na hili tutalishinda. Aidha, kwa yeyote anayetaka kusaidia, tunahitaji msaada wa maji na chakula kwa watu 500!” aliandika.
Zoezi la kudhibiti moto limekuwa likisimamiwa na Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi.