Eric Omondi amjibu Zuchu kufuatia ujumbe alioutuma kama maoni yake kwenye post aliyoiweka kupitia ukurasa wa mtandao wa Instagram wa mchekeshaji huyo maarufu wa nchini Kenya.

Post iliyokuwa na maneno yaliyosomeka ‘AMAPIANO Has Killed BONGO Flavour’ akimaanisha ‘Muziki wa Amapiano umeuua muziki wa Bongo Fleva’.

Ujumbe aliouandika kufuatia kukithiri kwa wasanii wa muziki wa Bongo Fleva kujikita katika kufanya aina ya muziki wa asili ya Afrika ya Kusini na kuuacha muziki wa asili ya Tanzania.

Muda mfupi baada ya post hiyo Omondi alipokea maoni (Comments) nyingi kutoka kwa wadau mbali mbali wa muziki Afrika Mashariki akiwamo Zuchu ambaye aliikosoa vikali kauli hiyo kwa kusema kuwa.

“Muziki wa Bongo fleva hauwezi kufa kamwe, wasanii wanatoka nje ya maeneo yao kutafuta utofauti. Kujaribu mirindimo mipya, hilo halijawahi kuua tasnia yoyote. Tasnia ya muziki ni kubwa sana wacha wasanii wajaribu mambo mapya ndio mabadiliko.”

Sasa punde baada ya Zuchu kuweka mtazamo wake huo, hatimaye mchekeshaji Eric Omondi amerejea na majibu akiyaelekeza kwa Zuchu kufuatia alichokiandika kwenye post yake iliyotangulia kwenye mtandao wa Instagram.

“Dada yangu mpendwa, hivi ndivyo inavyoanza, kila mara huwa tunaanza kwa kupoteza uhalisia na utambulisho wetu na kutoa visingizio vyake. Huku Kenya tulianza vivyo hivyo na Muziki wetu ukapotea, Wazungu wanasema “Kama haijavunjwa, usiirekebishe!!.

Bongo Fleva iko sawa kabisa na hakuna haja ya kuwacha Bongo Fleva ati Kwa ajili ya ku ‘Diversify’.

Amapiano ni Basi tu linalopita ila sisi tukipanda bila kujua linaenda wapi basi tutashindwa kurudi nyumbani.Tutakua tunauza sera zao na Tamaduni zao na Kuua chetu.

Unapoimba ‘Sukari’ kwenye hiyo Sweet Authentic Bongo Tone and Beat, unachofanya kimsingi ni Kuinua taifa na bendera ya Tanzania na TUNAIPENDA SANA na tunajivunia.

Lakini when you Continually replace that Bongo Sound na Amapiano baada ya Muda tutakuwa tumejipoteza. Niamini, hii ilitokea kwa muziki wa Kenya, I am Speaking from Experience.

Msalimu sana Kaka yangu na wana WCB wote waambie Nawapenda. Naja Dar January nitawaalika show yangu hapo Mlimani City.” Aliandika Eric Omondi.

Ni kwa kipindi cha takribani mwezi mmoja sasa, tangu mchekeshaji huyo wa Kenya kuanzisha Kampeni maalum yenye lengo la kuunyanyua muziki wa nchini Kenya kwa kupinga muziki wa wasanii wa mataifa mengine kupewa nafasi kwenye vyombo vya habari zaidi ya wasanii wazawa wa taifa hilo.

Kwa alichodai kuwa wasanii wa Kenya wamenyimwa thamani wanayostahili na wasanii wa nje ya Kenya ndio wanaopewa nafasi zaidi kitu kisicho sahihi na kwa mara ya kwanza tangu Kampeni hiyo ianze, Eric Omond ameamua kuoaza sauti kuhusu muziki wa Bongo fleva ambao asili yake ni nchini Tanzania.

Defao afariki Dunia
Peter Banda kuiacha Simba SC