Faiza Ally ambaye ni mzazi mwenza wa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu ameshambuliwa vikali baada ya kuweka kwenye mtandao video ya mtoto wao inayodaiwa kumdhalilisha mbunge huyo.

Katika video hiyo aliyoipost kwenye akaunti yake ya Instagram yenye wafuasi zaidi ya 236,000, Faiza anasikika akimwambia mwanae anaelia machozi kuwa amtumie ujumbe baba yake akiomba pesa ya kusuka kwa kuwa yeye ameishiwa pesa.

Kuisindikiza video hiyo iliyosambaa kwenye mitandao, Faiza aliandika ujumbe ambao umewaudhi wengi, “Anae mjua baba wa huyu mtoto amwambie analilia kusuka….. Anaomba baba yake amtumie hela kwa kuwa sina mawasiliano nae hopeful mtamfikishia ujumbe….. Na mimi ndio hivyo tena leo sina chapaa.”


Wafuasi wake waliporomosha lugha kali na zenye ukakasi, huku nyingine zikiwa matusi ya wazi wakimshambulia mrembo huyo. Kulingana na ukali wa lugha hizo, Dar24 imeamua kuziweka kapuni. Tunakuachia mdau ufikirie uhalali wa tendo alilolifanya mama huyu  wa mtoto mmoja.

Chenge aeleza atakachofanya endapo Escrow itajadiliwa tena bungeni
Picha: Mbuzi ajiunga Rasmi na Jeshi la Uingereza na Kupiga gwaride