Muungano mpya wa kuuza bidhaa za umeme nchini Tanzania umetangazwa hii leo kati ya Kampuni ya MeTL Group na Panasonic Life Solutions unaolenga kuangazia maisha katika Ulimwengu bora.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa masoko wa MeTL, Fatema Dewji hii leo Septemba 7, 2022 na kudai kuwa wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii katika kipindi cha miezi michache ili kuweza kupata mafanikio.

Amesema, “Tupo tayari kusonga mbele na mradi huu mpya wa kusisimua na ninaikaribisha timu kutoka Panasonic ili kutengeneza ulimwengu bora kwa wananchi kwa kusimamia maisha bora na ulimwengu bora.”

Bi. Fatema ameongeza kuwa, muungano huo pia unakusudia kwenda sambamba na kauli mbiu zote mbili, ambazo zinagusa maisha ya ya watu moja kwa moja hivyo kuleta ufanisi wa lengo lililokusudiwa.

Akiongea katika ukaribisho huo, Mkuu wa biashara ya mauzo ya bidhaa toka Panasonic Life Solutions India, Vishal Nangalia San amesema wanayo furaha kushirikiana na MeLT Group katika kufanikisha malengob ya muungano huo wa kibiashara.

Kenya: Jaji Mkuu amtaja Mungu hukumu ya kupinga matokeo
Waziri Mkuu aahidi makubwa kwa Wananchi