Mwaka mmoja baada ya kuwepo mgogoro mkubwa kati ya waimbaji wa nyimbo za injili, Flora Mbasha na Emmanuel Mbasha waliotuhumiana kwa usaliti umekamilika kwa wawili hao kurudisha upya mapenzi yao.

Mgogoro wa wawili hao ulifikia hatua kubwa ambapo Emmanuel Mbasha alifunguliwa kesi ya kumbaga shemeji yake (mdogo wake Flora), kesi ambayo ameishinda hivi karibubuni na mahakama kumuacha huru.

Siku chache baada ya uamuzi wa mahakama, Flora ametangaza rasmi kufuta kesi ya talaka aliyoifungua dhidi ya mumewe, lengo likiwa kurusha uhai wa ndoa yao yenye watoto wawili kwa kuwa bado anampenda mumewe huyo.

“Ninachoweza kusema ni kuwa yule ni mume wangu bado ninampenda. Tunamshukuru Mungu kwa hilo na kila mmoja amekuwa na amani ndani ya moyo wake,” Mbasha aliiambia Ayo TV.

“Nitaendelea kumpenda siku zote, he is my husband, I love him, I will always love him.” Alliongeza Flora.

Nasri: Hata Baba Yangu Akiwa Kocha Sirudi
Rihanna Mabusu Tele Na Kijana Huyu Mdogo