Hatimaye Rihanna ametua tena mikononi mwa kijana mdogo mwenye umri wa miaka 23, rapa Travis Scott (II) baada ya mihangaiko mingi katika mahusiano ya mapenzi na mastaa mbalimbali wakiwemo Drake na Chris Brown.

Tetesi za uhusiano kati ya Rihanna na Travis zilifika kileleni juzi (Oktoba 5) baada ya wawili hao kunaswa na kamera za paparazzi wakiwa katika Night Club moja jijini Paris Ufaransa ambapo walijiachia na kumwagiana mabusu bila kuficha.

Riri 2

Ripoti za Paparazzi waliohudhuria katika Night Club hiyo zinaeleza kuwa wakati wanacheza pamoja kwa mahaba kama njiwa katikati ya umati, Rihanna mwenye umri wa miaka 27 alikuwa akimbusu Travis shingoni, na Travis hakuwa analaza damu naye alimwaga mabusu shingoni na mabegani kwa mrembo huyo.

Riri

Umri sio kitu bali ni tarakimu tu, Rihanna anaonekana kuzama kweli kwenye penzi la Travis. Tetesi za uhusiano wao zilianza mwezi uliopita. Wiki hii walienda jijini Paris, Ufaransa kwa ajili ya kuhudhuria ‘Fashion Week’.

Flora Mbasha na Mumewe, Mapenzi Kama Zamani
Lowassa Ageukia Mikopo Ya Vyuo Vikuu, Atangaza Neema Kwa Wote