Imethibishwa rasmi kuwa wababe wa mapigano, Floyd Mayweather na Conor McGregor watapigana Juni 10, mwaka huu katika ulingo wa masumbwi.

Mmarekani anayefahamika kama ‘The Money’ na raia wa Ireland anaejulikana kama ‘Notorious’ wameuteua ukumbi wa T-Mobile Arena mjini Las Vegas kuwa sehemu ya pambano lao.

Kila mmoja ametaja bei yake ya kupandia ulingoni kuwa dola za Kimarekani Milioni 100, ingawa kiuhalisia McGregor atatakiwa kushusha bei ili kuhamishia ujuzi wake wa UFC katika ndondi.

Mayweather amesema, amereje arasmi ulingoni kwa ajili ya McGregor baada ya kustaafu akiwa amepigana mapambano 49 na kushinda yote rekodi sawa na ya gwiji, Rocky Marciano na hilo litaitwa “Pambano la Karne”.

Awali, ilionekana kama pambano hilo limeshindikana, hali iliyopelekea McGregor kuhamishia mpango huo kwa Manny Pacquiao aliyeupokea kwa mikono miwili, lakini sasa inaonekana kama Pacquiao amewekwa kando rasmi.

Mayweather anaonekana kulikamia pambano hilo akisisitiza kuwa hataki tena kusikia McGregor anaweka kikwazo chochote au kisingizio chochote bali kinachotakiwa ni kutwangana tu ili ijulikane nani mbabe zaidi.

PSG Wamshtaki Mwamuzi Deniz Aytekin
Video: Undani kutimuliwa Simba, Madabida, JPM amshtua Lema