Bodi ya wakurugenzi wa klabu ya Inter Milan, italazimika kusubiri hadi mwanzoni mwa juma lijalo ili kufanya maamuzi ya kusitisha mkataba wa meneja wa kikosi chao Frank de Boer.

Leo jioni kikosi cha Inter Milan kinatarajia kucheza mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Italia (Serie A) dhidi ya Torino, ikiwa ni siku tatu baada ya kupoteza dhidi ya Atalanta kwa kufungwa mabao mawili kwa moja.

Matokeo mabovu yanayomuandama meneja huyo kutoka nchini Uholanzi, yamekua kichocheo kwa viongozi kufikiria kumtimua na kufungua ajira kwa wengine ambao watawania kiti chake klabuni hapo.

Kwa sasa Inter Milan ipo katika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka nchini Italia (Serie A), ikiwa imeshuka dimbani mara 9 na kupoteza michezo 4 huku wakishinda 3 na kudroo mara 2.

Mwishoni mwa juma hili kikosi cha Inter Milan kitakabiliwa na mchezo mwingine wa ligi kuu ya Italia (Serie A) dhidi ya Sampdoria, na huenda matokeo ya mchezo huo yakatoa mustakabali wa De Boer.

De Boer aliajiriwa klabuni hapo mwanzoni mwa mwezi Agosti.

Siri Za Yanga Na George Lwandamina Zaendelea Kufichuka
Eric Bailly: Nitaimiss Man Utd Na Timu Ya Taifa Langu