Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kwa kuahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni 700 za kuendeleza ujenzi wa kituo cha afya kilichopo Kata ya Muriet jijini humo.
Ameyasema hayo wakati wa kumnadi mgombea wa udiwani katika Kata hiyo, Francis Mbise ambapo amewataka wananchi wa kata hiyo kumchagua diwani huyo ili aweze kuwaletea maendeleo.
Amesema kuwa amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kutoa msaada wa fedha hizo baada ya kuona juhudi kubwa alizozifanya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqqaro na mkurugenzi wa jiji hilo Athuman Kihamia ili kuleta maendeleo.
Hata hivyo, Gambo ameongeza kuwa fedha hizo zilizotolewa na Rais Dkt. Magufuli pia zitasaidia kujenga nyumba za polisi saba katika eneo hilo linalojengwa kituo cha polisi ambacho kitahudumia wananchi wa eneo hilo.
-
Video: Dkt. Shika kutumiwa mabilioni yake kutoka Urusi, ayalipia Bima
-
Dkt. Ndugulile alia na uhaba wa watumishi wa afya
-
Watendaji wa Serikali watakiwa kuzingatia mwongozo wa Bajeti