Watumishi wa kada mbalimbali katika sekta ya afya bado wanahitajika nchini ili kuboresha huduma ya afya kwa ajili ya kuokoa maisha ya watanzania ili kuifikisha nchi katika uchumi wa viwanda mpaka kufikia 2020.
 
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa mahafali ya pili ya chuo cha Afya na tiba cha KAM yaliyofanyika jijini Dar es salaam.
 
Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa wanakishukuru chuo hiko kwani wamekuwa na mchango mkubwa kwa kutoa rasilimali watu katika sekta ya afya kwani wametoa wataalamu wa afya wapatao 1600 mpaka hivi sasa.
 
“Tuna malengo ya kuwa na watumishi wa kada mbalimbali za sekta ya afya wapatao laki 1.849 na kati ya hao tumefanikiwa kuajiri watumishi 89842 na bado tunahitaji watumishi 95800 ili kuweza kuwa na rasilimali watu,” amesema Dkt. Ndugulile.
 
  • Wapangaji kulipa kodi ya mwezi mmoja
 
  • Balozi afunguka alivyomsafirisha ‘kijasusi’ Dkt. Shika
 
  • Wanaobeza viwanda mtazamo wao ni finyu- Mhagama
 
Amesema kuwa katika kupunguza vifo vya mama na mtoto Serikali kupitia Wizara ya afya imetoa shilingi milioni 700 kwa vituo vya afya ili kuweza kuboresha huduma za afya nchini.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafunzo na tiba dkt. Aloyce Musika amesema kuwa wahitimu wanatakiwa kujiendeleza na elimu ili kuongeza kiwango cha elimu na kuwa wabobezi katika kutoa huduma za afya zilizo bora na kwa uhakika nchini
Video: Waliofurika kumlaki Lowassa watawanywa kwa mabomu, Dk Shika aibua jipya, alipa dola 100
Watendaji wa Serikali watakiwa kuzingatia mwongozo wa Bajeti