Baada ya shambulio la kigaidi lililotokea Ijumaa usiku jijini Paris nchini Ufaransa, hali bado sio shwari barani Ulaya baada ya kuwepo kwa viashiria vya tukio jingine la kigaidi nchini Ubelgiji na kusababisha kuahirishwa kwa mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya Ubelgiji na Hispania uliotakiwa kufanyika leo usiku.

Mechi hiyo iliyokuwa ifanyike leo mjini Brussels Ubelgiji imeahirishwa saa 11 kabla ya mchezo kuanza kutokana na hali ya wasiwasi kushamiri nchini Ubelgiji huku ulinzi ukiwa bado hauja imarika sana na kwamba polisi wamemkamata mtu mmoja aliyekua katika vikundi hivyo vya kigaidi.

Pamoja na Hispania kuwa tayari kucheza mchezo huo, serikali ya Ubelgiji ilitoa ushauri wakutochukua uamuzi kwa kuuahirisha mchezo kwa sababu za kiusalama.

Account maalumu ya Twitter ya timu ya taifa ya Ubelgiji iliandika kutoa taarifa zaidi huku wakisisitiza kuwa ni busara kupokea ushauri wa serikali yao na kutofanya majaribio katika hali ya hatari.

Kwingineko, mchezo kati ya Ufaransa na England unachezwa kama ulivyopangwa jijini London huku manahodha wa England, Wayne Rooney na yule wa Ufaransa, Hugo Lloris wote wakisisitiza mchezo huo ni kuonesha kushikamana kwao na kwamba wako kinyume na magaidi.

Utafiti: Kujamiiana Kiasi Hiki Kutakuongezea Kinga Hii
Angela Merkel Kuwa Shuhuda Ujerumani Vs Uholanzi