Mshambuliaji wa klabu ya Sunderland Jermain Defoe ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England, kwa ajili ya michezo ya kimataifa ambayo itachezwa juma lijalo kwa mujibu wa kalenda ya shirikisho la soka duniani FIFA.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate, amemuita mshambuliaji huyo, kutokana na changamoto inayoikabili nchi hiyo kwa sasa ya kuwakosa Wayne Rooney na Hary Kane ambao ni majeruhi.

Kwa mara ya mwisho Defoe alijumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England mwaka 2013.

Southgate aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano wa kutangaza kikosi chake kuwa, hana shaka na mshambuliaji huyo kutokana na historia ya upachikaji wake mabao kujieleza yenyewe.

Msimu huu tayari Defore ameshaifungia Sunderland mabao 14 katika michezo 24 aliyocheza.

Mshambuliaji wa Man Utd Marcus Rashford naye ametajwa kwenye kikosi cha England.

Mbali na kuachwa kwa Harry Kane na Wayne Rooney kwa sababu za kuwa majeruhi, washambuliaji wengine kama Andy Carroll, Andre Gray, Troy Deeney na Daniel Sturridge hawakutajwa kwenye kikosi hicho.

England itacheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa soka duniani (Ujerumani) Machi 22, kabla ya kuwa wenyeji wa Lithuania katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 siku nne baadae.

Kikosi kamili kilichotajwa na kocha Southgate upande wa makipa

Fraser Forster (Southampton), Joe Hart (Torino) na Tom Heaton (Burnley)

Mabeki: Ryan Bertrand (Southampton), Gary Cahill (Chelsea), Nathaniel Clyne (Liverpool), Phil Jones (Man Utd), Michael Keane (Burnley), Luke Shaw (Man Utd), Chris Smalling (Man Utd), John Stones (Man City) na Kyle Walker (Tottenham)

Viungo: Dele Alli (Tottenham), Michail Antonio (West Ham), Ross Barkley (Everton), Eric Dier (Tottenham), Adam Lallana (Liverpool), Jesse Lingard (Man Utd), Jake Livermore (West Brom), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Nathan Redmond (Southampton), Raheem Sterling (Man City) na James Ward-Prowse (Southampton)

Washambuliaji: Jermain Defoe (Sunderland), Marcus Rashford (Man Utd) na Jamie Vardy (Leicester)

Mwalimu atiwa mbaroni kwa kumwadhibu mwanafunzi
Man Utd Yajisogeza Robo Fainali Europa League