Gavana wa Benki Kuu (BoT), Profesa Benno Ndulu amesema kuwa kuweka fedha kwenye akaunti maalum kwa lengo la kuzalisha (fixed deposit accounts) sio kosa kisheria.

Mchumi huyo ambaye pia alikuwa mjumbe wa Bodi ya TRA iliyovunjwa na Rais Magufuli hivi karibuni baada ya kukumbwa na sakata la kuweka fedha za umma kwenye fixed deposit accounts, alisema kuwa hakuna hasara ya kiuchumi kwa kuweka fedha hizo, lakini suala hilo lilifanywa kivingine.

“Kwani amesema fixed account zote ni mbaya, pamoja na za watu binafsi? Ndo hivyo sasa,” alisema Ndulu katika mkutano na waandishi wa habari jana uliolenga kueleza hali ya kiuchumi nchini.

“Ndio hivyo sasa. Nilijua mtanichomekea hilo kwahiyo nilikuwa tayari nimejiandaa,” aliongeza.

Rais Magufuli alisema kuwa alichukua uamuzi wa kuivunja bodi hiyo kwakuwa ilipitisha maamuzi mabovu ya Menejimenti ya TRA kuweka kwenye fixed deposit accounts za mabenki binafsi shilingi bilioni 26 zilizokuwa kwa ajili ya matumizi ya Mamlaka hiyo.

Rais Magufuli pia alitoa onyo kwa taasisi nyingine zinazofanya hivyo akiitaja Mamlaka ya Elimu Nchini (TEA) kuwa nayo imejihusisha na kitendo kama hicho.

#HapoKale
Tanzia: Mwanamapinduzi Fidel Castro afariki Dunia