Uongozi wa Klabu ya Getafe umetetea uamuzi wa kumsajili Mason Greenwood katika dirisha la usajili la kiangazi, ukidai Mshambuliaji huyo wa Manchester United hana tofauti na wachezaji wengine.

Greenwood alikamatwa na Polisi mwaka jana kwa tuhuma za kujaribu kubaka na kumshambulia mpenzi wake kabla ya mahakama kufuta kesi hiyo Februari mwaka huu baada ya mashahidi kujiondoa.

Kabla ya Getafe kumsajili Greenwood kwa mkopo alikuwa chini ya uchunguzi wa ndani uliosimamiwa na Man United kabla ya kutoa tamko rasmi kuhusu hatma yake, lakini baada ya miezi sita ya uchunguzi kukamilika uongozi wa klabu uliamua kumtoa Greenwood kwa mkopo akaanze maisha yake mapya nje ya England.

Kutua kwa Greenwood Getafe ilishtua Hispania hususan taasisi za kijamii huku wakiishutumu kutokana na uamuzi wao kabla ya utambulisho wake Jumatano (Septemba 06).

Hata hivyo, uongozi wa Getafe ulimkingia kifua kutokana na uamuzi wao wa kumleta mchezaji huyo wa kimataifa wa England ili kuimarisha safu yao ya ushambuliaji.

“Tulifanya kile tulichofanya, Tulimsajili Greenwood kwa sababu kulikuwa hakuna kizuizi,” alisema

mkurugenzi wa michezo wa Getafe, Ruben Reyes. Tumemsajili Greewood kama tulivyowasajili wachezaji wengine (Diego Rico na Oscar Rodriguez). Tulipaswa kufanya kazi yetu na hilo ndilo tulizingatia.”

Ripoti ziliripoti Man United iliweka kipengele cha kuvunja mkataba wa mkopo itakapofika dirisha dogo la usajili Januari hivyo kuna uwezekarno akarudi.

Young Africans kuzifuata Pyramid, Al Ahly
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 10, 2023