KAMPUNI ya Geita Gold Mine Limited (GGML), imeendelea kung’ara baada ya kuibuka mshindi katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara – Dar es Salaam maarufu kama sabasaba kwa kunyakua tuzo ya muajiri bora na msafirishaji bora wa madini nje ya nchi.

Pia GGML imepata tuzo ya mlipa kodi bora wa pili na muajiri bora anayezingatia taratibu za Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).

Tuzo zote zimetolewa Julai 13 na Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango na kupokewa na Mwanasheria Mwandamizi wa GGML, David Nzaligo kwa niaba ya uongozi wa kampuni.

Wa pili kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji.