Mshambuliaji wa klabu ya Rayon Sports ya nchini Rwanda, Jacques Tuyisenge, amesajiliwa na mabingwa mara kumi na tano wa ligi kuu ya soka nchini Kenya, (KPL) Gormahia.

Tuyisenge raia wa Rwanda, ambaye pia ni nahodha wa kikosi cha timu ya taifa ya Rwanda kwa wachezaji wa ndani “Amavubi”, anatarajiwa kujiunga na Gor Mahia baada ya kumalizika kwa fainali za mataifa bingwa ya Afrika CHAN ambazo zitaanza kuunguruma mwishoni mwa juma hili, jijini Kigali nchini Rwanda.

“Tumemsajili Jacques Tuyisenge ambaye atajiunga nasi baada ya kukamilika kwa mashindano ya CHAN hapo mwanzoni mwa Februari.” Katibu mkuu wa Gor Mahia, Ronald Ngala alinukuliwa na tovuti rasmi ya mabingwa hao mara kumi na tano wa KPL

Gor Mahia, pia wamekamilisha usajili wa kiungo Francis Kahata, na aliyekuwa mshambuliaji wa mahasimu wao wa jadi AFC Leopards, Jacob Keli akitokea kwenye klabu ya Nkana “Red Devils” ya nchini Zambia.

Keli amesajiliwa kwenye klabu hiyo, kama suluhisho la nafasi iliyoachwa wazi na mshambuliaji mzoefu Meddie Kagere.

Laurent Blanc Athibitisha Bifu Lake Na Cavani
Mexime: Mtibwa Sugar Hatuna Bahati Na Kombe La Mapinduzi