Mbunge kutoka chama cha upinzani nchini Zimbabwe, Eddie Cross amesema kuwa anaamini mke wa Rais Mugabe, Grace Mugabe, ametorokea Namibia baada ya kuwepo na hali ya wasiwasi.
Mwanasiasa huyo wa chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change (MDC) amesema kuwa anafahamu kwamba, Grace aliruhusiwa kuondoka nchini humo usiku wa kuamkia leo na jeshila nchi hiyo.
Ameongeza kuwa mke wa Rais Mugabe alikuwa hana sehemu nyingine ya kwenda kutafuta hifadhi baada ya kudaiwa kumdhalilisha mwanamitindo Afrika Kusini jambo ambalo lilimaanisha hatoweza kuomba hifadhi nchini humo kwani hatakuwa na usalama wa kutosha.
Aidha, katika taarifa rasmi kwenye televisheni ya taifa iliyotolewa na jeshi, Meja Jenerali, Sibusiso Moyo amelihakikishia taifa hilo kuwa rais na familia yake wako salama na usalama wao ulikuwa umehakikishwa.
Hata hivyo, Grace Mugabe amekuwa akitaka nafasi ya makamu wa rais kwa muda mrefu huku akimtaka mume wake, Rais Robert Mugabe kumtaja mrithi wake pindi atakapo maliza muda wake wa utawala.
-
Rais Buhari aunga mkono kufukuzwa kwa Walimu 20,000
-
Jeshi la Zimbabwe latoa sababu kuweka vifaru mitaani na Urais wa Mugabe
-
Jeshi la Zimbabwe lakanusha kufanya mapinduzi