Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amewaomba watanzania kumuombea yeye pamoja na familia yake kwa madai kuwa amekuwa akipokea vitisho visivyo na idadi.

Nyalandu ametumia ukurasa wake wa twittter ambao ameonyesha hofu yake na kusema kuwa vitisho visivyo na idadi vimekuwa vikimiminika ili kuhakikisha vinamnyamazisha.

“Napokea idadi isiyo ya kawaida ya vitisho tangu kuondoka CCM chama tawala. ni ajabu kuwa kuna hofu kubwa kutoka kwa wasomi, ambao wanatumia njia zote zinazowezekana kuninyamazisha,”ameandika Nyalandu

Aidha, amewaomba watanzania kwa ujumla kumuombea yeye pamoja familia yake ili kuondokana na vitisho anavyodai kutishishiwa ambavyo amesema vinalengo la kumnyamazima na kuzima harakati zake.

Hata hivyo, kabla ya kuhamia Chadema wiki kadhaa zilizopita, Nyalandu alikuwa Mbunge wa Singida Kaskazini na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM.

Grace Mugabe atimkia Namibia
Majaliwa aitaka wizara kufanya utafiti wa kina