Klabu ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani iko katika mazungumzo ya kumsajili kiungo wa Arsenal, Granit Xhaka, vyanzo vimeiambia ESPN.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake wa sasa na ingawa Washika Bunduki hao wana chaguo la kuongeza mwaka mmoja zaidi, vyanzo vinasema klabu hiyo bado haijakifikiria kipengele hicho.

Hilo limezua sintofahamu akilini mwa kiungo huyo juu ya mustakabali wake na Leverkusen imetafuta kufaidika kwa kuwafuata Arsenal na kuwapa ofa inayoaminika kuwa ya euro milioni 15.

Mkataba bado haujakamilika, lakini Xhaka yuko tayari kuondoka ikiwa Arsenal hawako tayari kumpa mkataba mpya wa muda mrefu zaidi.

Arsenal inataka kurekebisha safu yao ya kiungo msimu huu wa joto na imemlenga Declan Rice wa West Ham, ingawa mchezaji huyo wa kimataifa wa England huenda akagharimu pauni milioni 100 au zaidi.

Serikali kupitia maboresho sheria makosa ya kujamiiana
Simba SC yatakaa kumtoa Joash Onyango