Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, amejibu makombora aliyopigwa na Kada Mkongwe wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mzee Yusuf Makamba wakati akitoa neno juzi kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa CCM mjini Dodoma.

Makamba alisema kuwa Askofu Gwajima ni kiongozi wa dini aliyesema uongo dhidi ya Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho, Dk. Jakaya Kikwete aidai kuna mpango wa kukwamisha zoezi la kumkabidhi Uenyekiti wa chama hicho Rais John Magufuli na kwamba ameumbuliwa siku ile.

Akizungumzia kauli ya Mzee Makamba, Gwajima amesema kuwa yeye sio saizi yake hivyo haoni haja ya kumjibu, huku akirusha kijembe cha mafumbo kwa kutumia msemo wa kabila lake.

“Kule kwetu usukumani kuna usemi unasema ukikutana na mlevi, mzee na mgonjwa hutakiwi kumpiga unamuacha kama alivyo. Hivyo, mimi Makamba si saizi yangu namuacha kama alivyo na siwezi kumjibu,” Gwajima alimwambia mwandishi wa Tanzania Daima.

Mwezi uliopita, sauti ya Gwajima ilisambaa mitandaoni akisikika akidai kunasa mbinu za kutaka kukwamisha zoezi la kumkabidhi Rais Magufuli uenyekiti wa chama hicho, huku akimshauri kukihama na kuanzisha chama chake endapo mbinu hizo zitadhihirika. Kadhalika, aliukosoa utawala wa Serikali ya Awamu ya Nne uliokuwa chini ya Dk. Jakaya Kikwete kwa mafumbo mazito.

Gwajima alitafutwa na Jeshi la polisi kwa siku kadhaa kwa lengo la kumhoji lakini ilibainika kuwa alikuwa nje ya nchi. Jeshi hilo lilimkamata punde baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kiamtaifa wa Julius Nyerere. Askofu huyo alihojiwa kwa takribani saa tatu na kuachiwa baadae.

Auawa na chui punde baada ya kutoka kwenye gari
Terence Crawford amdunda Viktor Postol