Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ametoa agizo kwa kila halmashauri nchini kutoa hati zisizopungua mia moja kwa kila mwezi katika maeneo ambayo viwanja vyake vimepimwa.

Amesema kuwa hatimiliki za ardhi zisipotoka na kumilikisha kwa wamiliki wa ardhi migogoro haitaisha na matokeo yake ni kuwepo umilikishaji mara mbili (Double allocation).

Ameyasema hayo wakati akizungmza na watendaji wa sekta ya ardhi katika Mkoa wa Rukwa akiwa katika ziara ya kukagua utendaji kazi sekta ya ardhi nchini.

‘’kule ambako viwanja havijapimwa watendaji wake wanaweza kueleweka lakini mtu ana viwanja mia moja halafu anashindwa hati za idadi hiyo na wakati mwingine anatoa hati kumi tu huku akiwa amejiwekea lengo la kutoa hati mia moja,” Amesema Naibu Waziri Mabula.

Aidha Naibu Waziri Mabula amemuagiza Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoani hapo Swagile Mfinanga, kumpatia taarifa ya uandaaji hati kwa kila halmashauri yake kufikia mwisho wa mwezi wa nane.

Hata hivyo, hatu hiyo pia itafika mikoa yote kwa kuangalia idadi ya viwanja vingapi vimepimwa na wamiliki wangapi wameomba lakini hawajapatiwa na kama hawajaomba mara ngapi watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri husika wamekwenda kuahamasisha ili wamiliki waombe kupatiwa hati.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa Ardhi Mabula, amegawa Ankara za malipo ya kumilikishwa Ardhi kwa baadhi ya wananchi wapatao 593 waliopimiwa maeneo yao katika kata ya Momoka Manispaa ya Sumbawanga mkoa wa Rukwa.

Wanafunzi waliotuhumiwa kuchoma shule watiwa mbaroni
Simbachawene: Unatakiwa ujitathimini