Aliyekua mshambuliaji wa klabu ya Simba msimu wa 2015/16, Hamisi Kiiza yupo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa kijiunga na klabu ya Free State Stars inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa, Kiiza ambaye pia aliwahi kuitumikia klabu ya Young Africans, ameshamalizana na uongozi wa klabu ya Free State na sasa anasubiri kupata leseni ya uhamisho wa Kimataifa kutoka TFF.

Mshambuliaji huyo wa kutoka nchini Uganda anajiunga Free State kama mchezaji huru baada ya kutupiwa virago na klabu ya Simba ambayo iliingia mkataba wa miaka miwili na mganda huyo.

Kiiza ataungana na Mrisho Ngassa ambaye alijiunga na Free State Stars mwaka jana kwa mkataba wa miaka 4.

Arsenal Yamuweka Sokoni Jack Wilshere Kwa Masharti
Ukongwe Na Uwajibikaji Vyampa Heshima Wayne Mark Rooney