Muongozaji wa video za muziki, Hanscana ameelezea kile alichojifunza kutoka kwa waongozaji wa kimataifa ikiwa ni pamoja na wanachohitaji kukiona wasanii baada ya kulipia na kufanya video kwa gharama kubwa.

Hanscana amesema muongozaji nguli wa video kutoka Afrika Kusini, Godfather alimshauri kuwa kati ya mahitaji ya wasanii sio tu kupata video kali lakini pia kuhakikisha msanii anaonekana ‘mzuri’ anayevutia kwenye video hata kama ni mbaya kiasi gani.

“GodFather alinambia kwenye ‘video zako hakikisha unafanya mtu anaonekane mzuri. Hata kama ni mbaya vipi, hakikisha unamfanya aonekane cute. Kwa sbabu hata kwenye simu yake ana application zinazomfanya aonekane mzuri. Kwahiyo akitoka mbaya hatakuelewa kabisa,” Hanscana ameiambia Clouds TV.

Katika hatua nyingine,muongozaji huyo wa video za muziki nchini alisema kuwa tangu akutane na God Father na watayarishaji wengine wakubwa wan je ya nchi amejiongeza kwa kiasi kikubwa na kupelekea video zake kuchezwa kwa wingi kupitia vituo vya runinga vya kimataifa kama vile Trace.

Alisema kuwa tayari ameshaagiza vifaa vya kisasa vya kufanyia kazi kutoka Dubai na kwamnba baada ya muda mfupi watu wataanza kuona mabadiliko makubwa kwenye kazi zake.

Video: Seif awasha moto CCM, AFP wamtaka jaji Mutungi aifute CUF - Magazeti Juni 17 2016
Philip Mangula awajibu wanaodai CCM inahofu kumkabidhi Magufuli uenyekiti