Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesema kinasubiri Desemba 27, kifunge mlango ambao kimetoa kwa kwa wabunge wa viti maalum 19 akiwemo aliyekuwa mwenyekiti mwenyekiti wa baraza la wanawake (BAWACHA) kukata rufaa ya kupinga kuvulia uanachama wa chama hicho.
Mkurugenzi wa Itifaki, mawasilianao na mambo ya nje ya chama hicho John Mrema amesema kuwa wao wanasubiri disemba 27 kufunga mlango huo kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.
”Waulizeni wao wenyewe maana isiwe kama tunawalazimisha sisi tunachosubiri ni Disemba 27, tufunge mlango” amesema Mrema
Itakumbukwa desemba mosi Mdee na wenzake wakati wakiongea na waandishi wa habari walidai kupokea barua rasmi barua ya kuvuliwa uanachama huo Novemba 30 mwaka huu.
Ambapo walisema kuwa wataendelea kuwa wanachama wa hiari wa chama hicho kutokana na mapenzi waliyonayo kwa chama chao.
CHADEMA ilitangaza kuwavuaa uanachama wanachama wake 19 Novemba 27, baada ya kwenda bungeni kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalumu.