Hemed Phd amesema kuwa kupata mtoto na majukumu ya familia kuongezeka vilisababisha aweke kando kwa muda sanaa ya muziki na uigizaji.

Msanii huyo ambaye mara ya mwisho aliachia wimbo ‘Imebaki Story’ miaka miwili iliyopita amesema kuwa baada ya kupunguza kwa kiasi kikubwa majukumu ya kifamilia, ameamua kurejea kwenye ulingo wa sanaa.

“Sababu kubwa ni masuala ya majukumu ya kifamilia, kwasababu kwenye maisha inafika wakati sio muziki peke yake au filamu pekee, kuna watoto wameongezeka, kuna biashara inabidi nizisimamie,” Hemed aliiambia Clouds TV.

Msanii huyo ambaye ameachia wimbo wake mpya ‘Mkimbie’ amesema kuwa anatambua kwamba ndani ya kipindi alichokuwa kimya muziki umebadilika, hivyo amejipanga kuachia wimbo mmoja kila mwezi kufuta ukimya wake na kukabiliana na ushindani.

Kipaji cha Hemed kilianza kuonekana kupitia shindano la kuimba la ‘Tusker Project Fame’ lililokuwa linafanyika jijini Nairobi.

Uwezo wake ulizidi kuonekana baada ya kuanza kufanya kazi zake binafsi na kujihusisha na sanaa ya uigizaji.

Janjaro azungumzia mpango wa kutaka kujiunga na ‘Weusi’
Trump aapa tena kuiangamiza Korea Kaskazini