Kiungo mkongwe wa Mtibwa Sugar, Henry Joseph amewatakia kila kheri nyota waliondoka klabuni hapo na kuwaasa kuwa na nidhamu ya soka ili kuendelea kuwa katika ubora.

Wachezaji hao waliondoka klabuni hapo ni Muzamir Yassin, Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya na Andrew Vicent waliojiunga na timu kongwe za Simba na Yanga.

Nahodha huyo wa zamani wa klabu ya Simba na timu ya taifa ya Tanzania amewataka wachezaji hao kuwa na nidhamu, kujituma na kutolewa sifa ili waweze kuendelea na ubora wao kama ilivyokuwa msimu uliopita.

Henry Joseph

“Ni wachezaji wazuri na bado ni vijana kama wakitumia nafasi waliyoipata vizuri nina imani watafika mbali, kwa upande wangu nawatakia kila la kheri,” alisema Henry.

Aidha Henry amesema kukosekana kwa mawakala wa kutosha ndio kunachangia kukosa wachezaji wengi wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi ingawa kuna vijana wengi wenye uwezo.

Mtibwa ipo jijini Dar es Salaam na inafanya mazoezi yake katika Fukwe za Coco kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi.

Everton Wataja Bei Ya Romelu Lukaku
Manny Pacquiao afunguka kuhusu taarifa za kurudi ulingoni na kupumzika Useneta