Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeteketeza zaidi ya kilo 584.55 za dawa za kulevya zinazijumuisha kilo 569.25 za heroine na kilo 15.3 za cocaine zikiwemo tani mbili za bangi na mirungi.
Akizungumza kwa niaba ya Kamishina Jeneral wa Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Veronica Matikila amesema utekelezaji huu ni wakawaida na huwa unafanyika baada ya mashauri ya dawa za kulevya kukamilika Mahakamani.
”Dawa hizi amabzo zinateketezwa leo zinatoka katika Mahakama tofauti tofauti, Mahakama Kuu Kanda ya dar es Salaam lakini tuna baadhi ya dawa zinatoka Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi pamoja na Rushwa” amesema Veronica .
Kuna dawa zinatoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Pwani lakini pia tuna Mahakama za Hakimu Mkazi Kinondoni pamoja na Kigamboni na Mahakama ya wilaya Temeke”
Uteketezaji huo unaenda sambamba na ule uliofanyika februari 22, 2022 mkoani mtwara ambapo DCEA kwa kushirikiana na wadau mbalimbali iliteketeza jumla ya kilo 250 za dawa za kulevya zinazojumuisha kilo 51.7 za heroin.
Aidha amesema kuwa uteketezaji wa dawa hizo huwa unafanyika kwa uwazi mbele ya wadau wote muhimu wanaotambulika kisheria na kushuhudiwa na waandishi wa habari ili kuondoa dhana iliyojengeka kwa baadhi ya wananchi kwamba dawa za kulevya hukamatwa na hurejeshwa mtaani kuuzwa tena.
Uteketezaji wa dawa za kulevya ni kutekeleza amri ya Mahakama iliyotolewa katika kesi namba 2 ya mwaka 2018 kwenye kikao cha Mahakama Kuu kilichoketi mkoani Lindi mbele ya Jaji Latifa Mansour mwishoni mwa mwezi Oktoba na kumalizika Novemba 5, 2021.
Kwa mujibu wa Mamlaka ya Kudhibiti ba Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) zoezi hili limefanyika kwa mujibu wa kanuni namba 14 ya kanuni za kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya ya mwaka 2016 za Sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya ya mwaka 2015.