Mamlaka za Kiserkali nchini Argentina imesitisha sherehe zilizokuwa zikiendelea nchini humo za kusherehekea ushindi wa Kombe la Dunia kutokana na mamilioni ya watu kujazana katika mji Buenos Aires hali iliyopelekea kifo cha shabiki mmoja pamoja na majeruhi.

Sherehe za Ubingwa wa Kombe la Dunia zilianza rasmi nchini humo baada ya mchezo wa Fainali dhidi ya Ufaransa uliopigwa Jumapili (Desemba 18) nchini Qatar.

Mashabiki wengi wa Argentina walionekana kufurahishwa na Mafanikio ya Timu yao ya Taifa na walionesha kutojali hadi kufikai hatua ya kuipokea Timu yao Usiku wa manene ilipowasili mjini Buenos Aires jana Jumanne (Desemba 20).

Mbali na Mamlaka za Kiserikali kusitisha Sherehe hizo, pia Shirikisho la Soka nchini humo lilisitisha msafara wa basi la wachezaji na kuamua kuwapakiza katika helikopta kuwarudisha majumbani kwao.

Uamuzi huu ulifikiwa mara baada ya mashabiki wawili kujirusha kutokea juu ya daraja mpaka kwenye basi hilo ambapo shabiki mmoja alifanikiwa huku mwingine hakufanikiwa na hivyo alianguka mpaka chini.

Heroine, cocaine zateketezwa Dar
Kocha Geita Gold akataa kumwachia Saido