Mei 2 mwaka 2011, Kikosi maalum cha pili cha Makomando wa Marekani (SEAL Team 6) kilichokuwa Afghanistan kilitua katika maficho ya kiongozi na mwanzilishi wa kundi la kigaidi la Al Qaeda, Osama Bin Laden, mjini Abbottabad nchini Pakistani na kumuua kwa kumpiga risasi.

Osama alikuwa mtu anaetafutwa zaidi na Marekani akiwa hai au amekufa. Alihusika kuamrisha mashambulizi ya balozi za Marekani nchini Tanzania na Kenya, mwaka 1998, pamoja na kulishambulia jengo refu zaidi la Makao Makuu ya Ulinzi la Marekani (Pentagon), Septemba 11, 2001, siku ya Jumanne.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Ikulu ya Marekani, Osama alizikwa baharini kwa kufuata taratibu za dini yake  akiwa muumini wa imani ya Kiislamu.

Hata hivyo, kilichoshangaza dunia, ingawa tukio hilo lilishuhudiwa moja kwa moja na Ikulu ya Marekani ikiongozwa na Rais Barack Obama, picha za mwili wa Osama Bin Laden zimebaki kuwa siri nzito ya Jeshi la Marekani hususan kikosi kilichoongoza operesheni hiyo.

Ikulu ya Marekani ikifuatilia kwa karibu Operesheni ya iliyomuua Osama Bin Laden (2011)

Ikulu ya Marekani ikifuatilia kwa karibu Operesheni  iliyomuua Osama Bin Laden (Mei 2, 2011)

Maswali mengi yameibuka zaidi… kwanini mwili wa Osama ambaye alikuwa adui namba moja duniani wa Marekani, halafu habari njema ya kumuua imebaki kuwa na usiri wa picha ambazo ni ushahidi wa wazi wakati aliyekuwa Rais wa Iraq, Saddam Hussein alioneshwa moja kwa moja akinyongwa?

Hii inaweza kuwa siri ya kuficha picha hizo:

Matt Bissonnette, ambaye ni mmoja kati ya makomando wakikosi cha SEAL Team 6 kilichomuua Osama Bin Laden na walinzi wake wote ameandika kilichotokea kwenye kitabu chake alichokiita ‘No Easy Day’.

Bissonnette, ameeleza kuwa baada ya kumpiga risasi, wakati anahangaika kukata roho, walimshindilia risasi nyingi kifuani kwake na sehemu nyingine za mwili. Anaeleza kuwa waliutoboa vibaya mwili wa Osama na kuuvuruga akiwa sakafuni.

“In his death throes, he was still twitching and convulsing. Another assaulter and I trained our lasers on his chest and fired several rounds,” Bissonnette ameandika. “The bullets tore into him, slamming his body into the floor until he was motionless.”

BLD

Kwa namna alivyoelezea kwenye mahojiano mengine, inaonekana huenda Osama alipigwa karibu risasi 100 na makomando hao waliofanya mazoezi ya muda mrefu bila kujua wanaenda kumuwinda nani,  hadi dakika kumi kabla ya kutekeleza tukio ndipo walipojua ni Osama Bin Laden.

Kwa mujibu wa maelezo hayo, inasadikika kuwa huenda hii ni sababu muhimu iliyoifanya Ikulu ya Marekani hadi leo kutoruhusu kuoneshwa kwa picha za mwili wa Osama uliovurugika vibaya.

Lakini katika sheria ya vita, mwanajeshi ameruhusiwa kumpiga risasi adui aliyeanguka chini hadi atakapojihakikishia kuwa haleti madhara yoyote kwake.

“Pale ambapo adui hajasalimu amri, ni sahihi kwa askari jeshi aliye vitani kumpiga risasi kadhaa kadhaa chache kuhakikisha kuwa sio hatari kwake tena,” kimeeleza chanzo cha kuaminika cha mtandao wa businessinsider.

Imeelezwa kuwa huenda Marekani inahofia kukosolewa kwa kumpiga risasi nyingi ambazo hazikuwa na maana yoyote kijeshi.

“To do so would show the world a body filled with a ridiculous number of gunshot wounds,” mtandao huo umekinukuu chanzo chake.

Baadhi ya watu wamekuwa na shaka kama Osama Bin Laden aliuawa, lakini kifo cha Osama kilithibitishwa na uongozi wa kundi la Al Qaeda.

Juni 16, 2011, siku chache baada ya kifo cha Osama, Al Qaeda walimtangaza Ayman Al – Zawahiri aliyekuwa msaidizi wa karibu zaidi wa Osama kuwa kiongozi mpya wa kundi hilo la kigaidi.

Ayman Al Zawahiri

Ayman Al Zawahiri

David de Gea Na Chris Smalling Wang'ara Tuzo Za Man Utd
Mambo 10 Ya Ajabu Yaliyoizidi Kete Leicester City Kushinda EPL