Maziwa ni kinywaji na chakula kwa watoto wadogo, watu wazima na wagonjwa, maziwa ni moja ya vyakula vichache ambavyo ni mlo kwa sababu ya ubora wake wa virutubisho vilivyopo.
Wataalu wa Afya na wauzaji wamaziwa wamekuwa wakieleza faida za kadha wa kadha za uywaji wa maziwa Je? umewahi kujiuliza hasa ni faida gani hizo zitokananzo na unywaji wa maziwa.
Unywaji wa maziwa huondoa msongo wa mawazo: unashauriwa kunywa bilauri 1 ya maziwa ya uvuguvugu hii husaidia katika kuondoa msongo katika misuli na neva zako za fahamu.
Huzuia maumivu wakati wa Hedhi: wanawake wengi wnakabili wnaa maumivu wakati wa hedhi, utumiaji wa maziwa umethibitishwa kupunguza maumivu haya kwa kiasi kikubwa.
Unywaji wa maziwa hujenga misuli; maziwa yana mchango mkbwa katika ukuaji wa misuli hii ni kutokana na protini zinazopatikana katika maziwa, wanaridhia wengi hunywa maziwa mara baada ya mazoezi hii ni kwaajili ya kuupa mwili virutubisho kwaajili ya kujijenga tena.
Hupambana na maradhi mengine: kwa miongo kadhaa tafiti zimebaini kuwa utumiaji wa maziwa huzuia magonjwa mengi kama vile shinikizo la damu na kiharusi, inaaminika kuwa maziwa hupunguza lehemu mwilini na kuongeza uwezo wamacho kuona.