Mbunge wa Tandahimba, Katani Hamad Katani ameitaka Serikali kusimamia bidhaa na pembejeo za kilimo ili waannchi na wakulima waweze kunufaika na kilimo.

Katani ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma ambapo ameiomba Wizara ya Kilimo kusimamia na maslahi ya wakulima

”Mimi niombe kwanza Wizara ya fedha mpo hapa, hapo mnaposema single digits kwenye bidhaa hizi za kilimo pembejeo na vitu vingine muende mkasimamie Waziri bashe uende ukasimamie hayo maporojo yako utakuwa na vision kubwa utakuwa na mission kubwa kwa trade tunayokwenda hapo huwezi kwenda kufanikiwa nakwambia kaka angu”.

Mbunge wa Tandahimba Katani Hamad Katani

“Na nimesema hapa 2025 ukipata tani laki saba za pamba mie Katani nabaki Tandahimba na ubunge wangu naucha hukohuko nakuahakikishia leo hapa kwa trade tunayokwenda nayo”

”Hivi nyie wabunge wenzangu mmewahi kulima kweli au nyie mnadhani garden mnazoweka nyumbani kwenu ndiyo kilimo kile, umeweka maua kidogo mnadhani ndiyo kilimo kile rudini mashambani sie tunapotoka wakulima mkajaribu kulima mtamtetea mkulima kwa uchungu kuliko haya tunayoyafanya leo”.

”Mheshimiwa Naibu spika, na hii bahasha itakwenda kukutafuna mission zako vision zako ziko vizuri sana. Lakini kama hutakuwa na mkakati dhabiti sababu fedha huna hapa unakaaa unajitete hela zinakuja ziko wapi? wakulima watalalamika hawa ziko wapi….ziko wapi mnatudanganya watu wazima hapa mfumo miezi sita hakuna cha mfumo hakuna cha nini semeni hela hatuna mnatudanganya mfumo.”

Mkulima akiwa shambani

”Waziri hapa amefanya kazi kubwa maminara mpaka kilimanjaro huko mfumo upi wa compyuta mnatudanganya mfumo tuambieni ukweli, tunataka tumsaidie Mama kila anayesiamama anaona kazi inayofanywa na Mheshimiwa Rais lakini nyie wasaidizi wake fanyeni tathimini ya kina mimi ninawaambia fanyeni thamini ya kina tunakwenda wapi”

”Mwigulu Kaka angu Rafiki yangu umetutukana wabunge sana mimi nakwambia umetutukana wabunge sana na unapaswa ukae utafakari utakako kaa hapa hakuna anayeweza kujadili waganga wa kienyeji hapa hamna haya tunayojadili ni maisha ya watanzania na tumeletwa bungeni tuwasaidie watanzania hata wanairamba kule wanataka uwasaidie watanzani.”

Serikali kuanzisha mfuko wa Mazingira
Serikali yazitaka Halmashauri kutenga fedha matumizi ya ardhi