Serikali imezitaka Halmashauri za Wilaya zote nchini, kutenga fedha kila mwaka katika bajeti zao kwa ajili ya kuandaa Mipango ya Matumizi bora ya ardhi kwenye maeneo yote ya vijiji.

Wito huo, umetolewa jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Festo Dugange wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kaskazini, Francis Ndulane aliyetaka kujua ni lini serikali itatekeleza mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt. Festo Dugange.

Amesema, Halmashauri hizo pia zinatakiwa kuweka kuweka alama zinazoonekana kwa urahisi, ili kuweka alama zitakazokuwa zikilinda ardhi hiyo na kuzuia muingiliano wa matumizi.

Aidha, ameongeza kuwa Serikali imejipanga kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi ya vijiji sita kwa kila mwaka, ili kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara.

Hivi nyie wabunge wenzangu mmewahi kulima: Katani
Serikali yabainisha mikakati kupambana na Fistula