Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amebainisha mikakati ya Wizara ya kupambana dhidi ya ugonjwa wa Fistula, ikiwemo kutoa elimu dhidi ya mimba za utotoni na kuwaelemisha akinamama kuhudhuria kliniki mapema.

Dkt. Mollel, ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Aleksia Kamguna na kuongeza kuwa Wizara ya Afya imeendelea kutoa elimu kwa wajawazito kujifungulia katika vituo vya huduma, ili kuwahi kupatiwa msaada kama kutatokea tatizo la uchungu pingamizi au jingine..

Amesema, “Katika kupambana na ugonjwa huu wa Fistula Serikali imekuwa ikitoa elimu kuhusu mimba za utotoni kupitia elimu ya uzazi kwa vijana na kuwaelemisha akinamama kuhudhuria kliniki mapema, Serikali imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu na huduma katika vituo vyote nchini vya kutolea huduma za afya.

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel.

Amesema, kiasi cha shilingi Bilioni 1.3 kwa kimetolewa kwaajili ya upanuzi wa miundombinu ya majengo ya huduma za Dharura, Huduma za Wagonjwa Mahututi, Huduma za Mionzi katika hospitali ya Rufaa ya Morogoro.

Hata hivyo, Dkt. Mollel amesisitiza kuwa, tayari ununuzi wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi bilioni 1.8, umefanyika katika hospitali hiyo huku kiasi cha shilingi Milioni 350 kikitolewa kwaajili ya umaliziaji wa jengo la upasuaji wa mifupa (Orthopedic theatre) ambapo jengo hili litakamilika mwezi Juni, 2023.

Serikali yazitaka Halmashauri kutenga fedha matumizi ya ardhi
Mume ahoji uhalali kesi ya kumuua mkewe