Hospitali ya wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani inakabiliwa na changamoto ya ukosekanaji wa dawa pamoja na vifaa tiba ambavyo vinawapelekea wananchi wa eneo hilo kukosa huduma ya kupata dawa pindi wanapopelekwa katika hospital hiyo kwa matibabu.

Kukosekana kwa madawa na vifaa tiba imekuwa ni tatizo katika wilaya ya Bagamoyo na hivyo kupelekea wananchi wa chini wasiojiweza kukosa baadhi ya huduma za upataji wa dawa kutokana na kutokuwa na kipato kwa ajili ya kununulia madawa katika maduka makubwa mara baada ya kutoka hospitali kupima na kujua matatizo yanayowakabili katika miili yao.

Wakizungumza katika baraza la madiwani baadhi ya madiwani wamesononeshwa na kitendo hicho cha kukosekana kwa dawa muhimu katika hospital hiyo ya wilaya kitendo ambacho kinapelekea wananchi wa wilaya hiyo kupoteza maisha bila sababu.

Shumina Rashidi ni diwani wa viti maalum alisema kuwa wananchi wamekuwa wakipatwa na changamoto kubwa kwa kukosekana kwa madawa maalum ya binadamu kitu kinachopelekea kuwepo kwa sintofahamu kwa watu wa bagamoyo.

Aliongeza kuwa kukosekana kwa madawa katika hospital ya wilaya ya bagamoyo kunatokana na deni kubwa  ambalo wilaya hiyo inadaiwa na bohari ya madwa nchini (MSD) kiasi ambacho kilikuwa ni zaidi ya milioni 200 ingawa kwa sasa tumepunguza deni hilo na kubaki  kwa kiasi cha shilingi million 79.

“Kukosekana kwa madawa kunapelekea kuwapa tabu wananchi wa bagamoyo hivyo wananchi wamekuwa wakituuliza maswali mengi wawakilishi wao kuwa tatizo ni kitu gani kimepelekea kukosekana kwa dawa muhimu kwa ajili ya kutibu binadamu kitu ambacho kinahatarisha maisha ya wanabagamoyo” Alisema.

Kwa upande wake Abdul Mzee, diwani wa nia njema alisema kuwa hospitali ya wilaya hiyo imekumbwa na janga kubwa la kukosekana kwa dawa kutokana na deni kubwa kutoka katika bohari ya dawa (MSD) na hivyo kupelekea kutokupatiwa kwa dawa kutoka kwa wasambazaji wakuu wa dawa hapa nchini.

Aliongeza kuwa deni hilo limekwisha anza kushughulikiwa ili kuweza kuwasaidia wananchi wa wilaya hiyo ili waweze kupatiwa huduma sitahiki pasipo kuwepo na changamoto kwa wananchi hao.

“Kutokana na hali hiyo madiwani tumeamua kwa sauti moja kuhakikisha deni linalipwa ili kuweza kuwanusuru wananchi wa wilaya hiyo katika kuhakikisha huduma ya madwa inapatikana kwa wananchi wa bagamoyo”Alisema

Akizungumza katika hitimisho la kikao hicho kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo Violet Mlowasa alisema kuwa halmashauri imejipanga kuhakikisha changamoto hiyo inamalizika katika wilaya hiyo.

Aidha aliwataka wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kwani serikali ya wilaya imekwisha kufanya mazungumza na SMD juu ya kumaliza madeni waliyokuwa wakidaiwa na muda sio mrefu wataanza kuletewa dawa kama ilivyokuwa awali.

Kubenea kuondoka Chadema muda wowote
Walimu 7 wafutwa kazi, wengine walimwa barua