Hospitali ya Rufaa Kibena iliyopo Mkoani Njombe inakabiliwa na changamoto ya vifaa tiba kwa ajili ya kuwahudumia watoto Njiti pamoja na udogo wa chumba hivyo kusababisha mrundikano ambao umesababisha vifo kwa watoto takribani 80 kati ya 440 waliozaliwa mwaka jana.

Akizungumza na Dar24 Media ofisini kwake, kaimu mganga mfawidhi wa hospital ya rufaa Kibena, Dkt. Gaspa Kimaro amesema kuwa chumba kipo lakini ni kidogo kutokana na hospitali hiyo kupokea wagonjwa kutoka wilaya zote za mkoa huo na kwamba chumba hicho hakitoshelezi.

‘’Mama anashikwa na uchungu akiwa ajatimiza muda basi haraka sana wanamundikia rufaa na kuja hapa, kile chumba pamoja na udogo na idadi ya vitanda ni vitatu siku nyingine wanaingia watoto hadi 15 ambapo hulazimika kuwatoa na kuwachanganya na watoto waliozaliwa bila shida ambayo nayo ni hatari, kwa hiyo niseme tusingekuwa na hiki chumba tungepoteza watoto wengi zaidi’’amesema Dkt. Kimaro.

Naye muuguzi anayehudumia watoto Njiti katika hospitali ya Kibena, Isdora  Mwakinga amesema kuwa changamoto nyingine ni uhaba wa mashine ya kupumulia ambapo hulazimika kutumia mashine moja kwa watoto wanne.

Kwa upande wa Dkt. bingwa watoto hospitari ya rufaa Kibena, Erica Balama amesema sababu ya vifo kwa watoto Njiti kwa mkoa wa Njombe ni kutokana na kukosekana na vifaa vya na mahala pa kupatia huduma.

Mmoja wa wazazi aliyekuwepo hospitalini hapo, Elizabeth Sanga amesema ni vema mpango wa haraka ukafanyike ili kunusuru vifo kwa watoto hao kwani kuwachanganya na watoto waliozaliwa bila tatizo ni hatari.

 

Elimu yatajwa kuwa kikwazo kwa viongozi wa vyama vya ushirika
Wasichana wawaponda wazazi wao wakimtetea R Kelly, ‘baba ni tapeli’