Uongozi wa klabu ya Inter Milan umefanikisha azma ya kumfuta kazi Frank de Boer, ikiwa ni baada ya siku 85 za ajira yake kama meneja wa kikosi cha klabu hiyo.

Maamuzi ya kufutwa kazi kwa De Boer yamechukua mkondo wake na kukiacha kikosi cha Inter Milan kikishika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi ya nchini Italia (Serie A), baada ya kufungwa bao moja kwa sifuri dhidi ya Sampdoria mwishoni mwa juma lililopita.

Nafasi ya meneja huyo mwenye umri wa miaka 46, itashikwa kwa muda na kocha wa kikosi cha vijana cha Inter Milan Stefano Vecchi, na jukumu lake la kwanza litakuwa katika mchezo wa Europa League dhidi ya Southampton utakaochezwa kesho.

Mara baada ya maamuzi hayo kufanywa na viongozi wa Inter Milan, De Boer aliandika ujumbe katika mtandao wa kijamii wa tweeter “Kuendesha mradi kunahitaji muda wa kutosha ” Ninawashukuru mashabiki wote wa Inter Milan kwa ushirikiano mlionionyesha.

Kabla ya kujiunga na Inter Milan, De Boer alikuwa ameacha gumzo katika klabu ya Ajax baada ya kuiwezesha kutwaa ubingwa mara nne wa ligi ya uholanzi.

Mwezi Agosti De Boer alisaini mkataba wa miaka mitatu wa kuitumikia Inter Milan, akichukua nafasi ya mzawa Roberto Mancini.

De Boer ambaye alikuwa beki wa kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi, aliwahi kuhusishwa na taarifa za kusakwa na baadhi ya klabu za Everton na Southampton zote za nchini England mwanzoni mwa msimu huu.

Bunduki 11 za Ujangili zakutwa nyumbani kwa Mbunge
Arsenal, PSG, Bayern Munich Zatangulia 16 Bora Ulaya