Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi – CCM, Daniel Chongolo amewataka wananchi wa kata ya Masaka jimbo la Kalenga Mkoani Iringa kuacha kuwanywesha watoto ulanzi wapoenda nao shambani badala yake wabebe chakula kwa ajili ya watoto ili kuwasaidia kuondokana na tatizo la udumavu.
Chongolo amesema hayo wakati akizundua mradi wa bwawa la kuhifadhi maji uliopo kata ya Kasaka uliogharomu tsh Bilion 1.5 na kupanda vifaranga vya samaki 3000 na kuwataka wananchi kutumia bwawa hilo kuvua samaki na kutengeneza lishe bora kwa watoto na kuondokana na tatizo la udumavu.
Amesema, “Ni aibu unapopita barabarani wanasema watu wa Iringa wanaudumavu, ifike mahali tujikague tusiendelee na tabia ya kuwanywesha watoto ulanzi mnapoenda nao shambani muwabebee chakula,msiache watoto wakalelewa kienyeji,wakalelewa na ulanzi hakikisheni mnawapa chakula bora kwa sababu Iringa ni mkoa unaoongoza kwa kilimo.”
Aidha Chongolo ameongeza kuwa, Wananchi hao wanaweza kutengeneza mabwawa madogo madogo ya samaki kwa sababu ni muhimu katika lishe na wakumbuke kuwalisha watoto kwa sababu ni lishe muhimu.