Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amepongeza juhudi zinazoendelea kufanywa na Serikalichini ya Waziri wa Nishati, Januari Makamba na watendaji wote katika Sekta ya Nishati kwa kuendelea kuhakikisha watanzania wanapata nishati ya umeme ambayo pia inasaidia katika uboreshaji wa huduma za afya katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Waziri Ummy amesema hayo mara baada ya kutembelea banda la Wakala wa Umeme Vijijini – REA, kwenye maonyesho ya Wiki ya Nishati inayoendelea kufanyika jijini Dodoma katika viwanja vya Bunge.

Amesema, “upatikanaji wa umeme wa uhakika unasaidia pia katika kuboresha huduma za matibabu katika vituo vya kutolea huduma za afya hivyo kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa uharaka zaidi kwa kutumia vifaatiba.”

Katika maonesho hayo, badhi ya Wabunge na Mawaziri wametembelea mabanda mbalimbali ya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati, ambapo pia walipata maelezo ya kina kuhusu miradi mbalimbali ya nishati inayoendelea nchini.

Wanajihadi 35 wa kundi la IS wahukumiwa kifo kwa kupigana
Iringa wapigwa marufuku kuwapa watoto ulanzi