Mahakama nchini Libya, imewahukumu adhabu ya kifo wanajihadi 35 waliokutwa na hatia ya kupigana pamoja na kundi la Islamic State katika nchi hiyo iliyopo Afrika kaskazini.

Watuhumiwa hao, waliungana na IS wakati wa machafuko baada ya kuangushwa kwa utawala wa dikteta Moamer Kadhafi, wakiwa ni kundi la kwanza la wanajihadi 320 wanaodaiwa kuhusika na kundi la IS kufikishwa mahakakani na kuhukumiwa.

Mwaka 2015, Kundi la IS liliuteka mji wa kati wa pwani wa Sirte na kuweka ngome kabla ya kuondolewa mwaka unaofuatia na vikosi vinavyoitii serikali ya kitaifa iliyokuwa madarakani wakati huo, ambapo makao yake makuu yake yalikuwa mjini Tripoli.

Washtakiwa wengine 13, walihukumiwa vifungo vya maisha, baada ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa mwezi Agosti mwaka jana katika mji wa magharibi wa Misrata, ambao ni Wapalestina, Wasudan na Walibya na wote walikuwa wamewekwa kizuizini tangu Desemba 2016 na kukutwa na hatia ya kujiunga na kundi la kigaidi, pamoja na mauaji.

Mkutano wa dharula: Dkt. Mpango awasili Bujumbura
Waziri Ummy apongeza jitihada za Serikali sekta ya Nishati